Ukiwa na Nida tu umemaliza kila kitu

Mifumo binafsi, umma kuunganisha

DAR ES SALAAM: SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (HMTH) imesaini mkataba wa zaidi ya Sh bilioni 43.3 kwa ajili ya kusimika mitambo ya Tehama na kuziunganisha taasisi 661 kwenye mtandao wa pamoja.

Mkataba huo kati ya serikali na Kampuni za Soft net technologies Ltd na Emerging Communication Ltd umesainiwa leo Novemba 6,2023 jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekekezaji wa mradi wa Tanzania ya Kidijitali unaosimamiwa na Wizara hiyo ya HMTH.

Pia, serikali imezindua kikundi kazi cha Mapinduzi ya Kidijiti Tanzania, chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) ambalo Mwenyekiti wake ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji Saini sambamba na uzinduzi wa Kikundi, Mwenyekiti wa Kikundi hicho cha Kidijiti ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Abdullah amesema mkataba huo ni wa miezi 18 ambapo
zabuni hizo zinahusiana na usimikaji wa vifaa vya mtandao wa msingi (core network) kwa nchi nzima.

Amesema, mkataba huo utawezesha kufanikisha kituo cha uangalizi mtandao.

(network operation centre) na vifaa vya kuunganisha taasisi kwenye mtandao.

“Taasisi 661 zitaunganishwa ili kuziwezesha ziunganishwe katika mtandao wa Serikali (GovNET), mtandao huu umeunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano nchini.” Amesema Abdullah

Amesema, lengo ni kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa njia ya kidijitali.

“Wizaraya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na sekta binafsi,ipo katika mchakato wa kutengeneza mfumo wa kubadilishana taarifa kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi uitwao ‘Tanzania Enterprises Service Bus’,” amesema Abdullah.

Amesema, serikali inatarajia kuanzisha Mwananchi Portal,ambayo itajumuisha
kuweka utaratibu wa upatikanaji huduma zote zinazotolewa nchini.

“Hivyo nitoe wito kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa hii, ili umma wa watanzania uweze kupata taarifa ya aina ya huduma wanazozitoa kama taasisi kwa wakati na tija stahiki;”amesema.

Amesema, katika nyanja hizi za mabadiliko yakidijitali, serikali haina budi kuweka miundombinu thabiti ya teknolojiaili ili kuweza kufikia mapinduzi ya nne ya viwanda yanayoongozwa na TEHAMA.

“Misingi mikuu ya miundombinu hii ya kidijitali ni kuhakikisha tunakuwa na mifumo bora ya
utambuzi wa watu (Digital Identity),ujenzi wa mfumo wa pamoja wa malipo (DigitalPayment),na kuweka miundombinu rafiki na yenye usalama katika kubadilishana taarifa, ” amesema na kuongeza

“Kama taifa, lazima tujitoe kujenga bunifu za Kidijitiili kukabiliana na changamoto zinazoendelea katika nyakati hizi za mapinduzi ya kidijitali.

Amesema, Mifumo ya serikali na ya binafsi itakwenda kusomana, sasa hivi haisomani, ila itakapokamilika kuunganishwa, mtu akienda kufungua akaunti benki hana haja ya kubebe vyeti vya kuzaliwa, namba ya Nida tu inatosha akiingiza kwenye system kila kitu anakikuta huko.

” Amesema

Aidha, amesema pia itasaidia kupunguza vitendo vya rushwa kwani mtu hatokua na haja ya kumfuata mtu ili kupata huduma, kila kitu kitafanywa kwa njia ya mtandao.

Habari Zifananazo

Back to top button