Ukraine kujiunga EU

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenksy amesema nchi hiyo inakwenda kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya (EU).

“Ukraine itakuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya – Umoja wa Ulaya ambao utashinda.” amesema.

Akihutubia Bunge la Ulaya Mjini Brussels leo Februari 9, 2023 Zelensky ameushurukuru umoja huo kwa msaada wa silaha, vifaa vya nishati na mafuta pamoja na wanaoendelea kusimama na Ukraine kufuatia uvamizi wa warusi.

Advertisement

“Ukraine na EU wamefanya nguvu zao kuwa dhahiri kanuni na mbinu za juhudi sisi sote ni sawa.”amesema Zelensky.

Umoja wa Ulaya unajumuisha nchi 28, ambazo ni Austria, Belgium, Bulgaria, Croatia, Republic of Cyprus, Czech Republic, Denmark, Estonia, Finland, France, Germany, Greece, Hungary, Ireland, Italy, Latvia, Lithuania, Luxembourg, Malta, Netherlands, Poland, Portugal, Romania, Slovakia, Slovenia, Spain and Sweden.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *