Ukraine: Tutajibu kila shambulio la Urusi

TAIFA la Ukraine limesema itajibu kila shambulizi lililofanywa na Urusi tangu kuanza kwa vita vinayoendelea hivi sasa kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema mashambulizi ya Urusi ambayo yaliuwa watu wanane katika mji wa Kyiv na mmoja katika mji wa Zaporizhzhia hayatokaliwa kimya.

“Hakika tutajibu kila pigo kwenye miji yetu,” Zelenskyy alisema Jumatano. “Mashambulio yote ya Urusi yatapata majibu ya kijeshi, kisiasa na kisheria.”

Watu saba pia walijeruhiwa wakati mabweni mawili na chuo kimoja vilipopigwa katika mfululizo wa mashambulizi ya asubuhi na ndege zisizo na rubani kwenye mji wa Rzhyshchiv, kilomita 64 (maili 40) kusini mwa mji mkuu wa Kyiv, huduma za dharura zilisema kwenye Facebook.

Mtu mmoja aliokolewa kutoka eneo hilo na watu wanne waliaminika kuwa wamenasa chini ya vifusi. Shughuli za uokoaji zilikuwa zikiendelea Jumatano usiku. Mkuu wa polisi wa eneo hilo Andrii Nebytov alisema dereva wa gari la wagonjwa aliyekwenda eneo la tukio ni miongoni mwa waliofariki.

“Watu wengi kwenye mabweni waliokolewa kwa sababu walikuwa kwenye makazi ya mabomu,” Nebytov alisema. Saa chache baadaye, majengo mawili ya makazi yaliharibiwa katika shambulio la kombora katika mji wa Kusini Mashariki wa Zaporizhzhia. Mtu mmoja aliuawa na 33 walipelekwa hospitalini, maafisa walisema.

Zelenskyy alielezea shambulio la Zaporizhzhia kama kitendo cha “ukatili wa mnyama”. Aliongeza kuwa mashambulizi ya Jumatano yalionyesha Moscow haipendi amani.

Habari Zifananazo

Back to top button