Ukraine yatuma ‘drones’ 13 Moscow

URUSI imeishutumu Ukraine kutuma ndege zisizo na rubani ‘Drones’ 13 kwa lengo la kulipua baadhi ya maeneo katika mji Mkuu Moscow na jiji la Sevastopol.

Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Ulinzi nchini Urusi imeeleza ndege hizo ziliharibiwa huku zingine 11 zikiangushwa karibu na mji wa Sevastopol.

Uvamizi wa ndege zisizo na rubani unakuja siku moja baada ya Urusi kusema kuwa imedungua ndege mbili za kivita za Ukraine ambazo zilitumwa kushambulia Moscow, moja karibu na uwanja mkubwa wa ndege Kusini mwa mji Mkuu wa Urusi na moja Magharibi mwa mji huo.​

Mashambulizi ya anga ya Ukraine ndani ya Urusi yameongezeka tangu shambulio la kwanza la ndege isiyo na rubani kuripotiwa katika Ikulu ya Kremlin mwezi Mei.

Gazeti la New York Times liliripoti mwezi Mei kwamba mashirika ya kijasusi ya Marekani yanaamini kuwa majasusi wa Ukraine au ujasusi wa kijeshi ndio waliohusika na shambulio la awali la ndege zisizo na rubani kwenye Kremlin.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alionya mwezi uliopita kwamba “vita” vinakuja Urusi, na “vituo vya ishara na vituo vya kijeshi” vya nchi hiyo vikilengwa.

Habari Zifananazo

Back to top button