Ukweli wote kifo cha Askari aliyegongwa na gari

Kamanda asimulia

MWANZA: Kamanda wa Jeshi Polisi mkoani Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbrod Mutafungwa amewaongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa askari wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, WP. 3984 Sanjenti, Stella Alfonce (49).

Sanjenti Stella Alfonce alifariki Novemba mosi mwaka huu katika eneo la Nyamuhongolo kwa kugongwa na gari la shule ya Nyamuge ya jijini Mwanza akitekeleza majukumu yake ya kazi .

Ibada ya kuaga mwili wa askari huyo imefanyika katika Kanisa Katoliki Kigango cha Isegeng’he Parokia ya Nyakato Jijini Mwanza.


Kamanda Mutafungwa amesema uhai wa Stella umetoweka akiwa anatekeleza majukumu yake ya kusimamia sheria za usalama barabarani.

“Mwenzetu amefariki akiwa analitumikia taifa, tuna kila sababu ya kumuombea na kumkumbuka kwa ushujaa wake” amesema Kamanda Mutafungwa.

Habari Zifananazo

Back to top button