Ulega: Vijana wasifukuzwe kazi hovyo

WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametoa maelekezo kwa mameneja na wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu nchini kuhakikisha wanalinda na kusimamia maslahi ya watanzania waliopata fursa ya kuajiriwa na wakandarasi.

Ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati akikagua ujenzi wa miundombinu ya barabara ya mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Nne (BRT 4) sehemu ya Ubungo hadi Mwenge (km 13.5) na kupokea changamoto za vijana wa kitanzania kufukuzwa kazi wanapolalamika au kutotendewa haki ikiwemo kucheleweshewa stahiki zao na Mkandarasi China-Geo Engineering Corporation anayetekeleza mradi huo.

Ulega amesisitiza kuwa kijana akifanya makosa au ukiukaji wa sheria, hatua zichukuliwe kwa mujibu wa kanuni za kazi, lakini si kuwafukuza tu kiholela na kuiagiza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kufanya ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha vijana wanafanya kazi katika mazingira salama na yenye haki.

SOMA: Ulega ataka haki za wazawa miradi ya barabara

Aidha, baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo kipande cha Ubungo – Mwenge, ametoa miezi miwili kwa Mkandarasi China-Geo Engineering kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kama mkataba unavyosema na sio vinginevyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Ulega ametoa miezi miwili kwa Mkandarasi Shandong Luqiao Group anayejenga kipande cha Mwenge – Tegeta kuthibitisha uwezo wake wa kutekeleza mradi huo kwa kasi na ubora unaotakiwa na wakishidwa kutekeleza hilo Serikali itavunja mkataba na kutangaza zabuni upya ili kumpata Mkandarasi mwenye uwezo wa kukamilisha mradi huo.

Ulega amesema Mkandarasi huyo amekuwa akionesha uzembe na kutozingatia maelekezo ya Serikali licha ya kupewa muda wa kutosha kukamilisha mradi huo unaogusa maisha ya Watanzania moja kwa moja.

 

Amesisitiza Serikali haitavumilia mkandarasi yeyote anayeshindwa kutekeleza kazi zake kwa uadilifu, nidhamu na kasi inayostahili, hasa kwa miradi yenye umuhimu kama barabara zinazoelekea maeneo ya makazi na biashara.

Waziri huyo wa Ujenzi ameongeza kuwa serikali ina dhamira ya kuhakikisha miradi yote ya miundombinu ya barabara inakamilika kwa wakati ili fedha za wananchi zitumike kwa tija na kuleta matokeo yanayoonekana.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  2. Wamiliki wa Mabasi yaliokuwa yanaitwa Scandinavi – Watakiwa kuhudhuria Kikao cha Wadau wa Mabasi Nchini ili Kujua changamoto kwa nini mabasi yao hayaonekani Mtaani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button