Ulega Waziri Mifugo, Mwana FA awa Naibu Utamaduni, Michezo

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Februari 26, 2023 amefanya uteuzi pamoja na kuwahamishia majukumu mengine viongozi mbalimbali.

Rais Samia amemteua Hamis Mohamed Mwinjuma maarufu kama Mwana FA kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mwana FA anachukua nafasi ya Pauline Gekul ambaye amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Rais Samia amemhamisha Ridhiwani Kikwete kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Rais Samia amemteua Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi akichukua nafasi ya Mashimba Ndaki ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Deogratius Ndejembi amehamishwa kutoka kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi.

Dk Jimmy yonazi amehamishwa kutoka kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia na kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.  Nafasi hiyo imechukuliwa na Mohammed Abdulla Khamis.

Tazama teuzi nyingine chini.

Habari Zifananazo

Back to top button