HISPANIA; ULINZI mkali utaimarishwa kuelekea michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia taarifa ya chombo kimoja cha habari kilichoripotiwa kuunga mkono kundi la Islamic State kuchapisha taarifa za uwepo wa vitisho katika Jiji la Madrid.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) limesema linafahamu kuhusu vitisho hivyo, lakini michezo hiyo Arsenal na Bayern Munich, Man City na Real Madrid itaendelea kama ilivyopangwa.
Mawaziri wa Ufaransa na Hispania wamethibitisha kuimarishwa kwa hatua za usalama.
BBC wameripoti kuwa kituo cha vyombo vya habari kinachounga mkono IS kimechapisha mabango mengi yanayotaka mashambulizi katika viwanja vitakavyotumika michezo hiyo.