Ummy ataja vipaumbele Wizara ya Afya

DODOMA: SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imebainisha vipaumbele sita vya kisera katika sekta ya afya.

Akizungumza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema vipaumbele ambavyo vitawekewa mkazo zaidi katika kutekelezwa kwa mwaka 2024/25 ili kuendelea kuboresha huduma za Afya nchini ni pamoja na suala la bima huku kipaumbele namba moja akitaja kuwa ni rasilimali watu.

Pia, suala la ubora wa huduma za afya, utekelezaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote, wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika utoaji huduma za afya.

Habari Zifananazo

Back to top button