WAZIRI Wa Afya ,Ummy Mwalimu, amesema ni wakati sasa magonjwa ya afya ya akili kuingizwa katika mfumo wa bima ya afya, ili wananchi waweze kupata msaada wa kisaikolojia na matibabu ya afya ya akili.
Katika Kongamano la Kwanza la Afya ya Akili leo jijini Da es Salaam, Ummy pia alitaka uwepo wa huduma za afya ya akili na wataalamu kupatikana kuanzia ngazi ya zahanati hadi Hospitali ya Taifa na pia uwepo na vituo ambavyo watu watapata huduma hizo.
“Suala lingine nataka kujadili kwenye kuzuia ni kwa nini bima ya afya zisikubali kugharamia afya ya akili, kama tunaruhusu watu kwenda kwenye matibabu kwa nini huduma za kisaikolojia na huduma zingine za afya ya akili zisiwe kwenye huduma za bima ya afya?” Amehoji Ummy.
Amesema magonjwa ya akili yameongezeka, ambapo takwimu za kidunia zinaonesha kuwa katika ya watu nane mtu mmoja anatatizo la akili.
Ummy ameeleza kuwa magonjwa ya akili yaliyopo kwa kiasi kikubwa ni sonona, kihoro, sifenia, matumizi ya bangi ,pombe
Amebainisha kuwa watu Milioni 1.5 wanaishi na sonona wengi wao wakiwa ni wanawake.