WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu leo amewasili Mkoani Kagera kwa lengo la kujua hali inavyoendelea juu ya ugonjwa wa Marburg ulioibuka hivi karibuni mkoani humo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afyam, imeeleza kuwa pia Waziri Ummy amepokea taarifa kwa timu inayoongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, aliyoiagiza kuendelea kufuatilia ugonjwa huo mara baada ya kugundulika mkoni Kagera.
Wizara ya Afya ilitoa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa Marburg katika Wilaya ya Bukoka, mkoani Kagera ambapo watu watano wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
“Bado Serikali inatoa wito kwa Watanzania kuchukua tahadhari na kutoa taarifa endapo utapatwa na dalili kama za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi,” imesema taarifa hiyo.