Ummy: Kufanya mazoezi na mimi Ruksa!

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kama kuna Mtanzania anataka kushiriki mazoezi na Waziri wa Afya yuko tayari kuungana naye katika matembezi kila siku ya Jumamosi.

Ummy ameyasema hayo katika matembezi ya hisani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema anataka kuwatengeneza watanzania kuwa matajiri wa afya kwanza.

“Mimi ni mwanafunzi wa Prof Janabi na mmeona sasa nimeanza kupungua na nitaendelea kupungua kwasababu nazingatia,”amesisitiza Ummy.

Amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya afya, kuimarisha upatikanaji wa dawa,huduma za vipimo na rasilimali watu.

Ummy ameeleza kuwa kubwa zaidi watajikita katika elimu ya afya kwa umma ili wachukue tahadhari ya magonjwa yasiyoambukiza.

“Tunaona changamoto nyingi za magonjwa yasiyiombukiza watu wanatakiwa kuzingatia kinga kwa kuzingatia mtindo bora wa maisha kuliko kusubiri tiba ambayo ni gharama” amesema Waziri Ummy.

Habari Zifananazo

Back to top button