Ummy: Mataifa ya nje yavutiwa kutibiwa nchini

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema sekta ya afya imekua kwa kiwango kikubwa ndani ya miaka miaka mitatu  ya Rais Samia Suluhu Hassan kiasi cha kuvutia nchi nyingine nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kuja kutibiwa nchini ukilinganisha na miaka kadhaa iliyopita.

Ummy amesema sekta hiyo kwa sasa imejikita zaidi kwenye tiba za kisasa upande wa vipimo ambapo mashine za mionzi ya Citiscan zimeongezwa kutoka 13 hadi kufikia 45 nchi nzima.

Amesema, upande wa Ultrasound kwa sasa zinapatikana mpaka kwenye zahanati ambapo kabla ya Rais Samia kuingia madarakani kulikua na Ultrasound 476 na sasa zipo 665 kwa ajili ya mama wajawazito.

Advertisement

Upande wa mashine za moyo kutoka mashine moja mpaka mashine nne kwa sasa.

“Wagonjwa wa mataifa mengine wanakuja kupata huduma ya matatibanu hapa nchini ikiwemo nchi za Malawi, Uganda, Kenya, Comoro, Burundi na nyingine nyingi, hii ni hatua kubwa kwetu, ” amesema Ummy.

Aidha, Waziri huyo amesema magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Shinikizo la damu, Kisukari, Figo ndio yanayoongoza kuwa na wagonjwa wengi kutokana na tabia bwete.

“Nawaomba Watanzania kufanya mazoezi na kupunguza matumizi ya vyakula vya mafuta, Sukari na Chumvi ili kutunza afya zao zaidi, ” amesema Mwalimu.