UMMY: Toto Afya haijafutwa
WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza Toto Afya haijafutwa.
–
Ummy amesema kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili watoto kwa gharama ileile ya Sh 50,400 wakiwa shuleni.
–
Akijibu hoja za baadhi ya watu kwenye mtandao wa X leo Septemba 16, 2023 Ummy amesema kwasasa Toto Afya wamesajiliwa watoto 200,000 hivyo wazazi/walezi wahimizane kuwakatia bima ya afya watoto.
–
“Mwisho wa sera ya watoto wa umri chini ha miaka mitano au wasio na uwezo kupata msamaha bado haijafutwa, hospitali zote za umma ziendelee kuhudumia watoto umri chini ya miaka mitano.” ameleeza Ummy.