Ummy: Tumieni ARV kwa usahihi

DODOMA: WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amewataka watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kuzingatia  matumizi sahihi na endelevu ya dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI (ARV) ili kuendelea kujilinda na kuwalinda wengine.

Waziri Ummy ameyasema hayo katika kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania (NACOPHA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

“Nataka kuwasisitiza watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya dawa za kufubaza ugonjwa huo ili kujilinda nyie wenyewe lakini pia na kuwalinda wengine na ugonjwa huo”. Amesema Ummy

Aidha, amesema kuwa Jarida Maarufu la Kimataifa la Sayansi na Afya (Lancet) limethibitisha pasi na shaka ikiwa watu wenye virusi vya ukiwmi wakitumia vizuri dawa za ARV basi inapunguza maambukizi kwa wengine kwa asilimia zaidi ya 70.

“Kwahiyo niwaombe sana ndugu zangu wanaoishi na virusi vya ukimwi  tuendelee kuzingatie matumizi sahihi na endelevu ya ARV ili tuwakinge na wenzetu”. Amesisitiza

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button