UN kuipa Ghana Dola 500 SDGs

Umoja wa Mataifa umesaini makubaliano na serikali ya Ghana na kuahidi kuipa nchi  Dola milioni 500 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kuisaidia kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Ghana, Charles Abani amesema katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo kwamba, mkataba huo ni chombo muhimu zaidi cha kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo za Umoja wa Mataifa nchini Ghana.

Amesema, msaada huo mpya utawezesha taasisi na watu kujenga uwezo wao katika maeneo matatu muhimu.

Advertisement

Aametoa ufafanuzi zaidi akisema: “Maeneo hayo matatu muhimu ni mageuzi ya kiuchumi jumuishi, upatikanaji sawa wa huduma za msingi za kijamii na amani na usalama wa kudumu nchini Ghana na katika eneo hilo zima.”

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *