UMOJA wa Mataifa (UN) umewataka wabunge nchini Gambia kuondoa mswada unaoondoa marufuku ya ukeketaji wa wanawake.
Bunge la Gambia lilianza kuchunguza sheria hiyo siku ya Jumatatu.
Ukeketaji ulipigwa marufuku nchini Gambia mwaka wa 2015.
Hata hivyo, viongozi wa dini wenye ushawishi wamekuwa wakishinikiza marufuku hiyo ifutwe.
Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya robo tatu ya wanawake na wasichana wa Gambia wenye umri wa kati ya miaka 15 na 49 wamekeketwa.
Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa alisema mswada huo ni wa kuchukiza.