KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano nchini Sudan.
Antonio Guterres alizitaka pande zinazozozana kusitisha mapigano wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani ukikaribia.
Hatua hiyo inakuja wakati wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanajadili rasimu ya Azimio la Uingereza linalotaka kusitishwa mara moja kwa mapigano.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema kusitishwa kwa mapigano hayo kutasababisha kuisha kabisa.
Alionya kwamba mzozo wa kibinadamu nchini Sudan unafikia kiwango kikubwa na kwamba hali ya haki za binadamu inaendelea kudorora.