UNFPA kupunguza vifo wajawazito, watoto

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshighulikia Idadi ya Watu (UNFPA) limekabidhi magari saba kwa serikali lengo ni kusaidia programu ya kuboresha kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto mijini.

Magari hayo yanagharimu Dola za Marekani 250 sawa na Sh milioni 570 na yamekabidhiwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma pamoja na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu.

Akizungumza leo Juni 28, 2023 Dar es Salaam, mwakilishi mkazi wa UNFPA, Mark Shreiner alisema shirika hilo limewekeza kwenye mradi wa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto kama sehemu ya haki za binadamu akitakiwa kuishi.

Almesema mradi huo unalenga kuboresha hali ya afya ya uzazi katika mradi huo wa miaka mitano ukianzia mwaka huu hadi 2027 Kwa kuwa bado panahitajika kazi kubwa ya ufuatiliaji haswa katika afya mbalimbali za uzazi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa, Rehema Madenge amesema magari hayo yatawezesha usafiri kwa Dar es Salaam na Dodoma kwa kuwa eneo la vifo vya uzazi Kwa wanawake na watoto Bado linahitaji kufanyiwa kazi.

Amesema lengo la mradi huo kwa mijini ni kuwa na uzazi salama na hata kiwi kufa yoyote wakati wa kujifungua.” Mama hatakiwi kufa wakati wa ujauzito na kujifungua,chini ya mradi huo ni mama afike kituoni na kujifungua salama Kwa kuwa mimba sio ugonjwa,” amesema Madenge na kuongeza kuahidi magari hayo kutumika katika malengo tarajiwa.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button