UNFPA walia changamoto mtoto wa kike

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kwa kushirikiana na wadau wamejadili idadi ya watu duniani na namna ya kumsaidia mtoto wa kike kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo mkabili ikiwemo kupatiwa elimu ya afya ya uzazi ili kupunguza  vifo vinavyotokana na uzazi.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam, Meneja wa Programu ya Afya ya Uzazi-Mama na Mtoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA Tanzania), Felista Mbwana, wakati akielezea mkutano wa Idadi ya Watu Duniani na Maendeleo (ICPD25) unaotarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar Novemba 9 hadi 11, mwaka huu.

Amesema pamoja na juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali katika kuhakikisha vifo vya wajawazito vinapungua,  bado changamoto kubwa imeonekana katika vituo vya afya ambapo asilimia 90 ya vifo vimekuwa vikitokea huko.

Amesema kwa Tanzania hali ya vifo vya mama na watoto wachanga bado iko juu, kwani wanawake 556 kati ya vizazi 100,000 wanakufa kila mwaka kwa uzazi kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika.

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x