United, Arsenal zaidi ya mechi ya kirafiki

MAANDALIZI ya msimu mpya EPL yanaendelea kuchukua sura mpya, ambapo Manchester United na Arsenal zitakuwa uwanjani katika mchezo wa kirafiki utapigwa saa 6:00 usiku wa leo.

Timu zote zinaendelea kujiweka sawa kwenye usajili, hivyo mchezo huo utatoa nafasi kwa wachezaji wapya, lakini pia utatoa tathmini kwa makocha wa timu zote mbili namna ya kuuanza msimu mpya.

Wachezaji wapya ambao wanatazamiwa kuwepo kwa upande wa Arsenal, beki Jullien Timber aliyesajiliwa kutoka Ajax, Declan Rice kutoka West Ham United na Kai Havertz kutoka Chelsea, ingawa wote walipata nafasi mchezo uliopita dhidi ya MLS All Stars.

Kwa United tayari washakamilisha usajili wa Mason Mount kutoka Chelsea na kipa Andre Onana kutoka Inter Milan.

Habari Zifananazo

Back to top button