Spurs: Kane hauzwi

1494111655

KAMA ulidhani Manchester United itamsajili mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane kirahisi, achana na mawazo hayo, Mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs, Daniel Levy hataki kusikia habari hizo. Mirror wameripoti.

Kwa mujibu wa mtandao huo, Levy hataki kumuuza mchezaji huyo akiamini kuwa bado ana msaada na timu hiyo na ataendelea kusalia London.

United inahaha kutafuta mshambuliaji wa kati huku kukiwa na taarifa kuwa huenda wakaachana na Anthony Martial ambaye amekuwa akitumika katika nafasi hiyo.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *