United sasa nafasi ya tatu

Manchester United imepanda hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England, mara baada ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata katika mchezo wa raundi ya 18 dhidi ya Manchester City kwa kufikisha pointi 38, nyuma ya City wenye 39.

Man City walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Jack Grealish dakika ya 60 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Kevin De Bryune.

Dakika 18 baadaye, Bruno Fernandez aliisawazishia United, kabla ya Marcus Rashford kutundika msumari wa pili dakika ya 82 na mchezo kuisha na City kupoteza mchezo.

Advertisement

Man City sasa imepoteza michezo mitatu katika EPL, na baada ya kipigo cha leo imeendelea kuachwa na Arsenal kwa tofauti ya pointi tano, huku Arsenal ikiwa na mchezo mmoja dhidi ya Spurs kesho.