United watatoa £140m kwa Osimhen ?

PAUNI Milioni 140 inahitajika kwa klabu yoyote itakayotaka saini ya mshambuliaji, Victor Osimhen kutoka kwa mabingwa wapya wa ‘Serie A’ Napoli.

Manchester United ni miongoni mwa klabu inayopambana kupata saini ya Mnaigeria huyo, hivyo basi wametakiwa kutoa dau hilo. Mtandao wa Mattino via Mirror kutoka Italia umeripoti.

Wakati huo huo Napoli inaendelea kumsawishi beki wao wa kati Kim Min-jae kuongeza mkataba mpya ili aendelee kusalia klabuni hapo.

Bayern Munchen pia imehusishwa kutaka kumsajili mshambuliaji huyo, na kwa mujibu wa Daily Mail, nyota huyo ameonekana Berlin nchini Ujerumani, hata hivyo haukufafanua kinachoendelea nchini humo.

Habari Zifananazo

Back to top button