United yampa ulaji Luke Shaw

MANCHESTER United imetangaza kumpa mkataba mpya wa miaka minne beki wao Luke Shaw, mkataba utakaomuweka klabuni hapo hadi Juni, 30 2027.

Beki huyo ameichezea klabu hiyo mechi 249 tangu ajiunge nayo akitokea Southampton mwaka 2014. Ameshinda mechi 29 za kimataifa akiwa na England, akishiriki michuano ya Kombe la Dunia na Euro.

Luke Shaw alisema: “Miaka tisa iliyopita, nilisaini klabu hii ya ajabu, na ninafuraha kuongeza muda wangu wa kukaa. Nimekua sana tangu nije Manchester miaka hiyo yote iliyopita, kama mtu na kama mchezaji; Najua nini kinahitajika ili kufanikiwa katika klabu kama hii.

Advertisement

“Tuko mwanzoni mwa safari yetu chini ya meneja na wakufunzi wake. Tayari tumefanikiwa msimu huu, lakini tunataka mengi zaidi. Kuna fursa nzuri ya kuunda kitu maalum hapa, na nitatoa kila kitu kuwa sehemu ya hiyo.”ameongeza.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *