United yamtangaza Mount

Klabu ya Manchester United ‘The Red Devil’ imemtangaza kiungo mshambuliaji Mason Mount kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo akitokea Chelsea ‘The Blues’.

Mount amesaini mkataba wa miaka mitano utakaomuweka klabuni hapo hadi 2027, wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.

Advertisement

United imekamilisha dili hilo kwa uhamisho wa £55m ikiwemo add ons ya £5m.

“Nimefurahi sana kufanya kazi chini ya Erik ten Hag.

Si rahisi kamwe kuondoka katika klabu uliyokulia lakini Man Utd itatoa changamoto mpya ya kusisimua kwa msimu ujao”.

Amesema Mount.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *