Upatikanaji maji safi vijijini wafikia asilimia 79

DODOMA; SERIKALI imesema hadi kufikia Februari 2024, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini imefikia asilimia 79.6 ikilinganishwa na asilimia 77 Februari, 2023.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassum Majaliwa wakati akiwasilisha bungeni hotuba yake kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bungwa mwaka 2024/2025 leo bungeni mjini Dodoma.

“Vilevile, kwa upande wa mijini upatikanaji wa maji umefikia asilimia 90 ikilinganishwa na asilimia 88 Februari 2023.

“Mafanikio hayo yamechangiwa na kukamilika kwa utekelezaji wa miradi 374 inayonufaisha wananchi wapatao 2,274,193 wanaoishi vijijini pamoja na kukamilika kwa utekelezaji wa miradi 70 ya maji mjini,” amesema Waziri Mkuu.

Habari Zifananazo

Back to top button