Upelelezi kesi ya Chonji wakamilika

Upelelezi kesi ya Chonji wakamilika

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya kusafirisha Dawa za kulevya  inayomkabili mshtakiwa Muharami Abdallah (Chonji) na wenzake wane, umesema umekamilisha upelelezi wa shauri hilo na wanasubiri taarifa kutoka Mahakama Kuu, ili wawasomee maelezo ya mashahidi washtakiwa hao.

Hayo yameleezwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na Wakili wa Serikali, Caroline Matemu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio kesi hiyo ilipotajwa.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Abdul Chumbi, Rehani Umande, Tanaka Mwakasagule na Maliki Maunda ambao kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine na cocaine zenye uzito wa jumla ya Kilo 6.2.

Advertisement

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka imedaiwa kuwa Oktoba 21, 2014 katika eneo la Magomeni Makanya, Dar es Salaam washitakiwa hao walisafirisha gramu 5309.57 za dawa za kulevya aina ya heroine na katika shtaka la pili imedaiwa katika eneo hilo hilo walisafirisha dawa aina ya Cocaine zenye uzito wa gramu 894.28.

Washitakiwa hao wanaendelea kubaki mahabusu hadi Januari 18, 2023 kesi hiyo itakapotajwa tena.