Upelelezi kesi ya mmiliki Cambiasso wakamilika

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya, inayowakabili mmiliki wa Kituo cha michezo cha Cambiasso, Kambi Zuber na wenzake watano umedai kuwa  upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na washitakiwa  watendelea kubaki rumande hadi Januari 16 mwaka huu.

Wakili wa serikali, Caroline Matemu amesema hay oleo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio, anayeisikiliza kesi hiyo.

Advertisement

Matemu alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa idadi ya mashaidi na vielelezo.

Washitakiwa wengine ni aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya Simba Muharami Sultan, Maulid Zungu, Said Mwantiko, John Andrew na Sarah Joseph wote wakazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Katika shitaka la kwanza inadaiwa kuwa Oktoba 27, mwaka 2022 maeneo ya Kivule wilayani Ila, Dar es Salaam walikutwa na dawa za kulevya aona ya heroin zenu uzito wa kilogramu 27.10.

Katika shitaka la pili, washitakiwa hao wanadaiwa Novemba 4, mwaka 2022 maeneo ya Kamegele Mkuranga mkoani Pwani, walikutwa na dawa hizo zenye uzito wa Kilogramu 7.79.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *