“Uraia pacha unahitaji mjadala kitaifa”

Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea ripoti ya Kamati ya Kutathmini Ufanisi na Utendaji wa Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Kamati hiyo imesema suala la uraia pacha linahitaji mjadala wa Kitaifa ili kupata maoni ya Wananchi wote.

“Kwakuwa Serikali iliahidi kukamilisha mchakato wa hadhi maalum ili kukidhi shauku ya Diaspora Tanzania Kamati inashauri jambo hilo likamilishwe, hadhi maalum itatoa fursa kwa Diapora kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa na kupata haki ya kushiriki katika masuala ya kiuchumi na kijamii katika nchi yao ya asili.

Serikali iandae utaratibu wa kuelimisha umma kuhusu hadhi maalum na faida zake” “Kuhusu suala la uraia pacha maoni ya Kamati ni kwamba jambo hili linahitaji mjadala wa Kitaifa ili kupata maoni ya Wananchi wote.” Amesema Rais Samia.

Habari Zifananazo

Back to top button