Urusi kuisaidia nafaka Tunisia

URUSI imesema iko tayari kusambaza nafaka nchini Tunisia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Moscow, Sergei Lavrov alisema katika ziara yake, ambapo nchini hiyo ya Afrika Kaskazini inakabiliwa na uhaba wa chakula unaochochewa na ukame.

Katika mkutano na Rais wa Tunisia Kais Saied katika mji mkuu wa Tunis, Lavrov alisema mazao ya Urusi yamekuwa mazuri kwa mwaka wa pili au wa tatu mfululizo na kwamba iko tayari kusaidia Tunisia.

Lavrov alisema baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia Nabil Ammar kwamba “tulikubali kuendeleza ushirikiano wetu katika sekta zote.”

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Urusi alitaja maeneo ya kuahidi kwa ushirikiano wa nchi mbili kama vile kilimo, nishati, nguvu za nyuklia na teknolojia

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button