Urusi yaitisha Ukraine, yataka mazungumzo

Vita Urusi na Ukraine yaathiri biashara ya madini

URUSI imeitaka Ukrane kusalimisha maeneo yanayoshikiliwa na vikosi vya majeshi yake vinginevyo itaamua hatma ya ukrane wa namna wanayotaka wao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov ametoa kauli hiyo Jumatatu wiki hii kama sharti la mwisho la kutafuta suluhu huku akisisitiza Ukrane kufuata matakwa hayo kwa faida ya raia wake.

Kauli hiyo ni baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kutamka kwa mara nyingine kwamba yuko tayari kwa mazungumzo ya amani ambayo hata hivyo Marekani wanaona hayatafaa kitu katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

Advertisement

“Mapendekezo yetu yako wazi na yanatambulika na adui yetu, suala la kuachia maeneo yanayodhibitiwa na kuondoa vitisho vya kiusalama kwa Urusi,” Lavrov.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Rais Putin alisema Urusi iko tayari kwa mazungumzo huku akiilaumu Ukrane na washirika wa Magaharibi kwa kukwamisha mazungumzo hayo tuhuma ambazo Marekani wamezikanusha na kusema ni za uongo.

Vita hiyo ambayo imedumu kwa miezi kumi na moja sasa imekuwa ikichukua sura mpya kwa kadri inavyoendelea na kuacha maelefu ya raia wa Ukrane wakiteseka bila maji wala umeem kutokana na uharibifu wa miundombinu. Takribani raia milioni tisa wa Ukrane hawana umeme na wengine maelfu wameuawa wakiwemo wapiganaji wa vikosi vya pande zote mbili.