WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora, Jenista Mhagama, ameagiza mifumo iboreshwe mikoani kwa watu wanaomba ajira, badala ya kwenda Dodoma makao makuu kufanya usaili.
Amesema suala la umri wa watumishi wa umma kufanya kazi liendane na upandishwaji wa madaraja, lazima lifanyiwe kazi mwaka 2021/22, ili kila mtumishi apate stahiki zake sawa sawa na alivyoanza kazi.
Mhagama ameyasema hayo leo wilayani Arumeru, wakati akizungumza na watumishi wa umma katika ziara yake ya kikazi.
Amesema usaili wa maombi ya kazi unaofanyika Dodoma, utatumia gharama kubwa, hivyo lazima mifumo iimarishwe, ikiwemo kanzi data ya sekretarieti ya ajira nayo iboreshwe, ili kuongeza ufanisi na inapotokea nafasi ya kazi baada ya kutangazwa kwa nini msichukue aliyefaulu mwingine badala ya kutangaza.
Alisema wazazi wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kufanya usaili wa kazi, hivyo lazima gharama za wazazi au walezi zipungizwe, maana wanaoomba kazi ni wengi wanaopata ni wachache na hata wanokosa, ikitokea nafasi nyingine uhitaji wapewe sababu walifaulu, lakini nafasi za ajira ni chache