Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limetangaza kuwa kuanzia kesho Julai mosi, 2023 dirisha kubwa la usajili kwa msimu mpya wa 2023/2024 litakuwa wazi.
Taarifa iliyotolewa na TFF leo Juni 30, 2023 na kusainiwa na Ofisa Habari Clifford Ndimbo, imeeleza kuwa dirisha hilo litakuwa wazi hadi Agosti 31 , 2023.
“Hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili tafadhali zingatia muda huo wa usajili” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa dirisha dogo la usajili litafunguliwa Desemba 16, 2023 na kufungwa Januari 15, 2024.