HALMASHAURi ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, imetenga jumla ya Sh Millioni 20 katika bajeti ya mwaka 2022/2023 kwa ajili ya ukarabati wa barabara.
Hayo yamesemwa leo kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani, wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira, ambaye ni diwani wa kata ya Bukomela, Kulwa Shoto akiwasilisha taarifa juu ya kamati hiyo.
Amesema kuwa greda lilifanya kazi na kuharibika baada ya kutengeneza kilomita 21 na kwamba bado liko kwa fundi..
Diwani Viti Maalum, Ester Matone amesema kwa taarifa waliyonayo wameelezwa mtambo umeingiza kiasi cha Sh milioni 18.7, lakini matengenezo ya greda yametumia Sh milioni 4.5, hivyo wametaka greda hilo liwanufaishe sababu barabara wanaziona bado changamoto ya kutopitika.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Linno Mwageni amesema kulikuw na changamoto ya uaminifu kwa dereva aliyekuwepo, hivyo wamepata dereva mwingine anaamini mambo yatakuwa mazuri.