SERIKALI imehimiza matumizi ya mfumo wa kidigitali katika kusimamia vyama vya ushirika.
Hayo yamesemwa leo na Mrajisi wa vyama vya ushirika, Dk Benson Ndiege, wakati alipokuwa akikagua mabanda ya wana ushirika katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo duniani, ambayo maonesho yanaendelea katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Amesema mifumo ya kidigitali inasaidia kusimamia vyama vya ushirika kuondokana na changamoto zilizokuwa zikijitokeza kama ubadhirifu wa fedha.