Ushuru wa Shisha, Sigara wapaa

SERIKALI imekusudia kutoza ushuru wa bidhaa ya Sigara na Shisha kwa asilimia 30.

Katika bajeti ya serikali iliyowasilishwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba, serikali imependekeza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 30 kwenye Sigara na bidhaa za aina hiyo zinazotumia mbadala wa tumbaku zinazotambulika kwa Hs code 2402.90.00.

Mwigulu amesema pia tumbaku inayovutwa kwa kutumia bomba la maji inayotambulika kwa Hs code 2403.11.00 na Sigara za kielektroniki, Shisha na bidhaa za aina hiyo zinazotambulika kwa Hs codes 8543.40.10, 8543.40.90 na 9614.00.00

Advertisement

Amesema, lengo la hatua hiyo ni kujumuisha bidhaa mpya zinazotumika kama mbadala wa tumbaku ambazo pia zina athari sawa na tumbaku.

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *