Usiingie 18 za Man United Boxing Day

Ufalme umesimikwa miaka 31 iliyopita

MANCHESTER, England: WAKATI wengi wakiifurahia Boxing Day kwa kujionea zawadi walizopokea wakati wa Sikuu ya Christimas kutoka kwa wapendwa wao na wengine wakiitumia siku hiyo kuwatembelea wale wanaowapa thamani katika maisha yao kuna wengine siku hiyo imekuwa ya kipekee mno.

Tuitizame simulizi ya kusisimua ya Mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu ya England (EPL), Manchester United ambao wao wameamua kuitumia Boxing Day kusimika ufalme wao katika kandanda la England.

Achana na ushindi wa kibabe waliopata jana dhidi ya Aston Villa, kumbukumbu zinatusafirisha zaidi ya miaka 31 iliyopita ambapo rasmi tuliipata EPL, ndio ni mwaka 1992 historia mpya kwenye soka la England ilipoanza  baada ya utambulisho wa EPL.

Inafahamika kwamba katika kipindi hicho ndipo, Manchester United walipokuwa katika moja ya zama bora chini ya Kocha Sir, Alex Ferguson, Man United ya wakati huo ilikuwa ikitembeza dozi kwa yeyote anaekatiza kwenye 18 zao.

 

Mbali na mafanikio ya kunyakuwa mataji mbalimbali timu hiyo inashikilia simulizi maridhawa kuhusu Boxing Day kwani hii ndio timu pekee katika Ligi Kuu ya England iliyopoteza michezo michache zaidi Boxing Day, ipo hivi tangu mwaka 1992, United wamecheza michezo 28 siku moja baada ya Christimas na wameshinda michezo 22, vipogo michezo miwili pekee na sare katika michezo minne.

Katika  michezo hiyo miwili waliyopoteza mwaka 2002 walipotea mabao 3-1 kwa Middlesbrough  kisha wakafungwa mabao 2-0 na Stock City mwaka 2015, ushindi mkubwa zaidi  kwa Man united Boxing Day ulikuwa mwaka 2011 walipoitandika Wigan Athletic mabao 5-0.

Timu zilizopitia kikombe cha mateso zaidi kutoka kwa mashetani hao wekundu wa Manchester kwenye Boxing Day ni Newcastle United, Sunderland, na Everton waliopoteza michezo mitatu kila mmoja walipokutana na miamba hiyo.

Kudhihirisha hilo kizazi kilichopo ndani ya timu hiyo kilihakikisha rekodi pamoja na heshima inasalia wakilazimika kutoka nyuma mabao 2-0 na kuitandika Aston Villa mabao 3-2 na kuimaliza Boxing Day kibabe, lugha rahisi hapa ni kwamba licha ya ubora wa Aston Villa waliingia kwenye anga za United bila ruhusa yao.

 

Habari Zifananazo

Back to top button