‘Usikubali kufanyiwa ukatili kisa kulinda ndoa’

‘Usikubali kufanyiwa ukatili ili kulinda ndoa’

MWALIMU Veronica Kidemi, amewaasa wanawake kutovumilia ukatili wanaofanyiwa na wenza wao kwenye ndoa kwa kigezo tu cha kulinda heshima.

Ametoa kauli hiyo jijini Arusha, wakati alipokuwa akichagia mjadala ulioandaliwa na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambao unahusu ukatili wanaofanyiwa wanawake katika ndoa katika wiki ya Azaki 2022 jijini Arusha.

Amedai yeye binafsi alifanyiwa ukatili wa kukatwa kiganja cha mkono na mume wake, ambaye kwa sasa hayupo naye, sababu ikitajwa ni wivu wa mapenzi

Advertisement

Amedai hatasahau ukatili huo aliofanyiwa Septemba 26, 2020 na kusababisha kiganja chake kukatwa, hivyo kutoa rai kwa wanawake kutokubali vipigo, unyanyasaji wa mwili na kingono kwa kudhani wanapendwa huku wanapata ulemavu.

Veronica ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Kiranyi na Mkazi wa Kijiji cha Siwandeti, amedai alikuwa akipigwa na mume wake, wakati mwingine akimtukana.