“Usikubali wakuendeshe na wala usibishane nao”

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amempa mbinu za kufanya vizuri katika Mkoa wa Tanga mkuu mpya wa mkoa huo Balozi Batilda Burian mara baada ya kumuapisha kiongozi huyo.

Akizungumza katika hafla ya uapisho wa viongozi leo Ikulu Dar es Salaam Rais amesema hana mashaka na Balozi Batilda katika majukumu yake mapya.

“Balozi Batilda nimekupeleka Tanga kwa ulivyo hivyo nadhani utakwenda nao, Waziri alikuwa anatumia maguvu sana, sasa wewe na Tanga tulivyo nadhani utakwenda nao vizuri, usikubali wakuendeshe lakini usibishane nao, nenda kasimame nao vizuri” amesema Rais Samia.

Balozi Batilda Burian anachukua nafasi ya Waziri Kindamba aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART).

 

Habari Zifananazo

Back to top button