Usipomsindikiza mke kliniki faini sh 50,000

Ni mkakati kupunguza vifo vya wajawazito na watoto

KIJIJI cha Neruma wilayani Bunda mkoani Mara kimepitisha sheria ndogo inayowalazimisha wanaume kuwasindikiza kliniki wenza wao kipindi cha ujauzito.

Akizungumza katika mahojiano maalum na HabariLeo, Mtendaji wa Kijiji cha Neruma wilayani Bunda mkoani Mara, Mwalimu Kapei Laizer Lazaro anasema katika kikao cha wananchi kilipitisha faini ya sh 50,000 kwa mwanaume kutompeleka kliniki mwenza wake.

Pia, mwanamke akijifungulia njiani faini ni sh 50,000 na akijifungulia kwa Mkunga wa Jadi faini ni sh 200,000.
Amesema wameweka faini hizo ili kupunguza vifo vya wajawazito na Watoto ambavyo vimekuwa vikikithiri katika kijiji hicho kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchelewaji wa kuwahi kufika kituo cha afya, na kutohudhuria kliniki kipindi cha ujauzito.

“Hapa tuna kituo kikubwa cha afya cha Kasaunga ambacho kinahudumia vijiji vitano, kwa pamoja tumejiwekea sheria hii ili kuwahimiza wanaume kushiriki katika malezi ya Watoto kuanzia tumboni, kama mama anasahau kunywa dawa za kuongeza damu basi baba atamkumbusha, watapata pamoja elimu ya uzazi wa mpango na elimu ya lishe, hii inawasaidia katika ukuaji wa mtoto.”Amesema Laizer

Aidha, amesema wamekuwa wakitoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuwasaidia mabinti kuepuka mimba za utotoni na wale ambao tayari wamebeba mimba zisizotarajiwa wanapewa elimu ya uzazi wa mpango ili wasirudie makosa.

UTII WA SHERIA
HabariLeo inazungumza na kina baba ambao wamesindikiza wake zao kliniki na kugundua kuwa sio kliniki za ujauzito tu bali pia wanawasindikiza wenza wao kwenye kliniki za watoto.

Jerome Mwita, anamsindikiza mke wake kliniki wakati wa ujauzito wake akizungumza anasema “Unajifunza vitu vingi,” Mwita (29)

“Na kitu kingine, ni vyema kufanya hivyo, ni njia ya kutengeneza familia bora. Pia, napata uzoefu wa kutosha juu ya afya na makuzi ya mtoto.”Anasema

Lakini Mwita, mvuvi, anawezaje kutenga muda wa kufanya hivyo na wakati huo huo akaweza kuendelea na shughuli zake za kujipatia kipato?

HabariLeo ilitaka kujuwa, iikizingatiwa kwamba hii ni moja wapo ya sababu kubwa zinazotajwa na wanaume kutokuhudhuria kliniki.

“Hiki ni kitu cha muda; ninaweza nikapanga siku fulani napeleka mtoto kliniki na ikawa hivyo,” anasema Mwita, kijana mweusi na mwenye urefu wa makamo. “Kwa upande wangu, ningewashauri wanaume wenzangu wawe na tabia ya kuwasindikiza wake zao kliniki.”

BABA KAMILI

Mfungo Paul, baba wa watoto wanne anasema sheria iliyowekwa na Kijiji chake imemlazimu kujenga utamaduni wa kumsindikiza mke wake kliniki kila mara inapotokea haja ya kufanya hivyo na sasa kwamba kitendo hicho kinamfanya ajihisi kuwa baba kamili mwenye kutimiza wajibu wake.

“Kumsindikiza mke wangu kunaleta faida nyingi,” Mgungo, ambaye kitaaluma ni fundi mabomba, anasema “Nitakuwa najua nimeongezewa uzito wa majukumu yangu kama baba. Nitakuwa najua mke wangu anatakiwa kujifungua wakati gani ili nianze kujiandaa. Nitajua vitu gani hatotakiwa kufanya katika kipindi cha ujauzito.”

MUAMKO BADO MDOGO
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kasaunga, Dk Reuben Chenge anasema kwamba muamko bado ni mdogo sana miongoni mwa wanaume linapokuja suala hilo husika licha ya sheria kali zilizowekwa na wanakijiji.

Changamoto hiyo ni kubwa sio tu kwa kituo cha Kasaunga bali ni tatizo la nchi ambalo lilipelekea serikali kuandaa mpango maalumu wa kubadilisha hali ya mambo uliopewa jina la Mwongozo wa Kitaifa wa Ushiriki na Ushirikishwaji wa Wanaume Kwenye Masuala ya Afya ya Uzazi.

Wataalamu wanashauri wanaume wahudhurie kliniki ili waweze kupata elimu ya afya ya uzazi pamoja na malezi ya mimba hadi kujifungua, wakisema endapo kama wanaume watapata elimu hiyo itasaidia kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi. Pia, utamaduni huo unahusishwa na kujengeka kwa mahusiano mazuri kati ya baba na mtoto atakayezaliwa.

Kaimu Mratibu wa Huduma ya Mama na Mtoto Kituo cha Kasaunga wilayani Bunda anasema kwamba ni muhimu kwa vituo vya kutolea huduma kuwapa kipaumbele akina mama wanaosindikizwa na waume zao, akisema hatua hiyo itachangia kurekebisha hali ilivyo hivi sasa.

“Kwa nchi zetu ni kwamba ukimuambia baba aje hospitali, hakikisha hakai muda mrefu,” anasema.
“Hiyo ndiyo changamoto ambayo wanaume wengi wanapata, na haya mambo yanawezekana, hapa kwetu wanaume wanaoleta wake zao tunawapa kipaumbele na anapewa ratiba kwamba wewe utakuja saa tano. Saa tano anakuja, ndiyo muda wao. Wamekuja, wanapimwa, wanaondoka.” Anasema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
LynnStubblefield
LynnStubblefield
1 month ago

Earn money in USA, high scores from trusted resources. Work at your own pace. Regular Payments. Search in different job categories. Work anywhere on your vs03 computer, laptop or mobile phone. Update your profile at any time.
.
.
Detail Here————————————->>> http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by LynnStubblefield
Tamekaoodward
Tamekaoodward
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by Tamekaoodward
favem
1 month ago

My last paycheck was 11000 dollars .I simply work daily from home 3-4 hours and earn 95 bucks for every hours detail on Here….>
https://www.pay.salary49.com

money
money
1 month ago

WAZEE WA KULA JICHO HUWA MNATUMIA MBOOO SIZE GANI KUINGIZA KWENYE JICHO

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg

Capture.JPG
Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x