USITISHAJI vita wa muda kati ya Israel na Hamas umeingia siku ya tano na sasa zimeongezwa saa 48 kukubaliwa kwa mkataba huo.
–
Taarifa ya BBC imeeleza kuwa Wapalestina watatu wataachiliwa kutoka magereza ya Israel.
–
Kundi la jeshi la Hamas limesema haliwashikilii mateka wote katika Ukanda wa Gaza, na kwamba kufanya hivyo kunaweza kukwamisha kuwakomboa walio hatarini zaidi.
–
Mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7, yaliuwa takribani watu 1,200 na 240 kuchukuliwa mateka tangu wakati huo.
–
Wakati huohuo, Wizara ya Afya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema zaidi ya 14,500 wameuawa katika kampen ya Israel kulipiza kisasi.


4 comments