Utafiti kubaini maeneo yenye mafuta wakamilika

SINGIDA: MRADI wa kuchukua data za mitetemo za 2D katika kitalu cha Eyasi Wembere umefikia mwisho huku wataalamu wakieleza kuwa na matumaini ya utafiti huo kubainisha na kuainisha maeneo yenye viashiria vya uwepo wa rasimali ya mafuta.
Hayo yamebainika hivi karibuni wakati wa ziara ya ufuatiliaji iliyofanywa na Maafisa wa Mamlaka ya udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) katika eneo la Eyasi Wembere mkoani Singida ambapo mradi huo umekuwa ukitekelezwa.
Bei za petroli, dizeli zapungua
Akizungumza na maafisa hao Mjiofizikia wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Meneja Mradi huo ,Sindi Maduhu alieleza kuwa utafiti huo wa 2D umefanyika katika maeneo yaliyopo katika Wilaya sita zilizo ndani ya Mikoa mitano ambayo ni Singida, Arusha, Tabora, Shinyanga na Simiyu.
Akieleza historia fupi ya utafiti wa mafuta kwenye bonde hilo la Eyasi Wembere Maduhu alieleza kuwa utafiti ulianza mwaka 2015 kwa kuchukua taarifa za kijiofizia (gravity magnetic) ili kubaini ukubwa wa eneo la bonde na kuangalia kina cha miamba tabaka iliyopo katika eneo husika.
Eneo la Eyasi Wembere lina kilometa za mraba 10630, na utafiti huo ulilenga kusoma aina na kina cha miamba ili kubaini uwezekano wa uwepo wa mafuta au gesi asilia katika eneo husika.
Utafiti katika bonde hilo umekuwa ukiendelea kufanyika kwa vipindi tofauti tofauti na kwa kutumia teknolojia mbalimbali ambapo kufikia mwezi Julai 2023 utafiti wa data za mitetemo kwa njia ya 2D ulianza rasmi kwenye eneo hilo.

Akizungumzia ushiriki wa wazawa kwenye mradi huo, Maduhu alisema Watanzania wengi wamenufaika na nafasi za ajira katika kipindi chote cha utekelezaji mathalani mwaka 2022 zaidi ya Watanzania 40 waliajiriwa kwa ajira za muda ili kufanya kazi ya kukusanya taarifa za kijiokemia.

Aidha amebainisha kuwa tangu kuanza utafiti wa 2D mwezi Julai, zaidi ya Watanzania 250 wamepata ajira katika mradi huo huku takribani asilimia 98 ya kazi za kitaalamu zikifanywa na wazawa ikiwa ni pamoja na kazi za kuendesha mitambo huku ikilinganishwa na asilimia 2 pekee iliyohusisha raia wa kigeni.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work AT Home
Work AT Home
1 month ago

Earn money in USA, high scores from trusted resources. Work at your own pace. Regular Payments. Search in different job categories. Work anywhere on your vs03 computer, laptop or mobile phone. Update your profile at any time.
.
.
Detail Here———->>> http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Work AT Home
Gloria Richardson
Gloria Richardson
Reply to  Work AT Home
1 month ago

I’m making $90 an hour working from home. I never imagined that it was honest to goodness yet my closest companion is earning 16,000 US dollars a month by working on the connection, that was truly astounding for me, she prescribed for me to attempt it simply. Everybody must try this job now by just using this website.. http://Www.Easywork7.com

Last edited 1 month ago by Gloria Richardson
HayleyMelinda
HayleyMelinda
1 month ago

[ JOIN US ] I am making a good salary from home $16580-$47065/ Dollars week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. ( 99q) I thank God every day I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started.…………> http://Www.SmartCareer1.com

Garages&ServiceStations
Garages&ServiceStations
1 month ago

PATA HUDUMA YA MATENGENEZO YA MAGARI KWA MATATIZO YOTE GARI YAKO NA POPOTE ULIPO TANZANIA

NA

MOVABLE KURASINI GARAGE SERVICE STATION

Address: Dar Es Salaam,

,Post Office box: 21493,

Phone number:

022 285 1500

Categories: Garages & Service Stations.

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.jpg

– PIGA SIMU TUKUHUDUMIE

Garages&ServiceStations
Garages&ServiceStations
1 month ago

PATA HUDUMA YA MATENGENEZO YA MAGARI KWA MATATIZO YOTE GARI YAKO NA POPOTE ULIPO TANZANIA

NA

MOVABLE KURASINI GARAGE SERVICE STATION

Address: Dar Es Salaam,

,Post Office box: 21493,

Phone number:

022 285 1500

Categories: Garages & Service Stations..

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.jpg

– PIGA SIMU TUKUHUDUMIE

Back to top button
5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x