Utafiti kuleta majibu matumizi bayoteknolojia ya kisasa Tanzania

KATIKA miongo mitatu iliyopita kumekuwepo na maendeleo ya kasi kwenye matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa ambayo yameleta athari chanya kwenye sekta za kilimo na afya ya binadamu na wanyama.

Ili kuongeza tija kwenye sekta za uzalishaji na huduma kwa jamii, serikali iliandaa na kuweka bayana Sera ya Taifa ya bayoteknolojia ya mwaka 2010, Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 na Mfumo wa Taifa wa Usimamizi wa bayoteknolojia ya Kisasa wa mwaka 2005.

Mfumo huu unajumuisha Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 iliyotanguliwa na Sera ya mwaka 1997, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004 pamoja na miongozo na kanuni za kusimamia matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa za mwaka 2009 na kama zilivyorekebishwa mwaka 2015 ili kuwezesha utafiti kufanyika nchini. Kwa kuzingatia umuhimu huo, Februari 12, mwaka jana Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango alizindua sera hiyo mpya ya Mazingira ya Mwaka 2021 jijini Dodoma.

Advertisement

Akizungumza na HabariLEO, Naibu Katibu Mtendaji wa Chama cha bayoteknolojia Tanzania (BST), Dk Nicholas Nyange anaelezea tafsiri ya bioteknolojia ni mbinu inayotumia mifumo ya kibaiolojia ya viumbe hai kutengeneza, kuboresha bidhaa au michakato kwa ajili ya matumizi maalumu.

Aidha, “bayoteknolojia ya kisasa ambayo pia inajulikana kama uhandisi jeni au mabadiliko ya kijenetiki (GMO) ni mbinu inayohusisha kuhamisha jeni ama kinasaba kinachobeba sifa inayohitajika kutoka kiumbe kimoja kwenda kingine na kupata kiumbe kilichoboreshwa kijenetiki,” anasema.

Anasema matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa ni mikakati ya kuhakikisha utafiti na matumizi ya bidhaa zitokanazo na viumbe vilivyoboreshwa kijenetiki hazileti madhara kwa binadamu, wanyama au mazingira.

Dk Nyange anasema bioteknolojia ya kisasa inadhibitiwa kuhakikisha teknolojia hiyo au bidhaa zake hazileti madhara yoyote kwa binadamu, wanyama au mazingira kama ilivyoainishwa katika Mfumo wa Taifa wa Matumizi Salama ya bayoteknolojia ya Kisasa unaosimamiwa na kuratibiwa na Idara ya Mazingira ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini unakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo kusababisha ukuaji mdogo na usio na tija.

Anataja changamoto hizo ni kuongezeka kwa joto, ukame na kuongezeka kwa ardhi yenye tindikali kunakosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Pia kuongezeka kwa magonjwa na wadudu waharibifu wa mimea, JADIDAAA Jengo la Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dar es Salaam. kwa ajili ya majaribio ya bioteknolojia kwa kushirikiana na SUA,” alisema Bashe.

Aliongeza: “Lazima tuijue, hatuwezi kujua kama miaka 20 ijayo dunia itatulazimisha na wanafunzi wanasoma, wanamaliza hatuwezi kuikataa hii sayansi.” Bashe alisema Rais Samia Suluhu Hassan katoa fedha za utafiti, bajeti ya utafiti ikichukua Tari na Wakala wa Uzalishaji wa Mbegu (ASA) kwa jumla ilikuwa ni Sh bilioni 15 na zimeongezeka.

Naye Mhadhiri wa SUA, Dk Philbert Ninyondi alinukuliwa akisema Tanzania imekuwa ikifanya uamuzi wa kutumia au kutotumia mazao na bidhaa za GMO kwa taarifa za mapokeo.

Dk Ninyondi anasema sayansi ya uhandisi jeni iko wazi haina mmiliki ila usalama wa taifa unawekwa njia panda ukizuia utafiti. “Marekani inaongeza kuwekeza kwenye utafiti huo.

Nchi za Asia kama China zinafanya utafiti wa GMO. Wale wanaotaka GMO, wote wanahitaji utafiti. Kutokana na sababu hizo, taifa letu linahitaji utafiti kumaliza ubishi wa GMO,” anasema Dk Ninyondi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI), Patrick Nguediagi amempongeza Bashe kwa kuruhusu utafiti huo kuendelea ili taifa lisiachwe nyuma na kujua kinachoendelea.

Kwa upande wake Dk Daba Tadessa kutoka Ethiopia, anasema uboreshaji wa kijenetiki ni moja kati ya mbinu ya kibaiolojia inayosaidia viumbe hai au mbegu za mmea kuongeza sifa zingine ambazo hawajazaliwa nazo mfano sifa ya kumudu wadudu na magonjwa.

“Hakika, hii teknolojia imekua zaidi duniani ikiwemo Afrika kwa sasa. Kwenye chakula teknolojia hii inapita kwa njia za kawaida na kemikali za mmeng’enyo wa chakula na kufyonzwa kama protini au chakula kutokana na sehemu ilipotokea,” anasema Dk Tadessa.

uhaba wa aina bora na zilizothibitishwa za mbegu zenye kutoa mavuno mengi na zenye kustahimili kasi ya mabadiliko ya tabianchi yaani ukinzani dhidi ya magonjwa, wadudu waharibifu na kustahimili ukame.

Anasema wakulima wengi wameendelea kutumia mbegu zisizo na ukinzani kwa magonjwa na wadudu waharibifu hivyo kulazimika kununua na kutumia viuatilifu kwa wingi kwa ajili ya kupata mavuno ya kutosha.

“Hii imeongeza gharama za uzalishaji, kupunguza tija na kumletea mkulima madhara kiafya. Matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa yanaweza kutupatia suluhisho katika changamoto zilizoorodheshwa,” anasema Dk Nyange.

Anasema tathmini ya hivi karibuni ya matumizi ya teknolojia hiyo duniani inaonesha mazao yatokanayo na uhandisijeni yameongeza kipato na kuboresha maisha ya wakulima. Dk Nyange anasema kilimo cha kutumia mazao yatokanayo na teknolojia hiyo ya kisasa kimesaidia kupunguza matumizi ya viuatilifu, kuhifadhi mazingira na kupunguza gharama za uzalishaji.

Pia anasema mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa yaliyoongezewa virutubisho vya vitamini A na madini ya chuma yanayochangia katika kulinda na kuboresha afya za wakulima na walaji.

Anasema Afrika nchi tatu zilizonufaika na kilimo cha mazao yaliyoboreshwa kwa kutumia teknolojia ya uhandisi jeni ni Afrika Kusini wanakolima pamba, mahindi na soya hekta milioni 2.9, Burkina Faso zao la pamba hekta milioni 0.3 na Sudan pamba hekta milioni 0.2.

Anasema utumiaji wa teknolojia hiyo umechangia manufaa makubwa kwa mkulima kwa kuwa baada ya Sudan kuanza kutumia teknolojia hiyo mavuno ya pamba yaliongezeka kutoka wastani wa kilo 1,000 kwa hekta hadi kufikia kilo 2,500. Hivi karibuni nchi za Malawi, Kenya na Ethiopia zimeanza kilimo cha pamba itokanayo na teknolojia hiyo.

Takwimu zinaonesha asilimia 80 ya pamba yote inayolimwa duniani ni pamba ya teknolojia hiyo. Anasema nchi nyingi za Afrika zimepiga hatua kwenye utafiti wa mazao ya chakula na biashara, ikiwemo Nigeria iliyofanya utafiti wa muhogo, mahindi, pamba na kunde, Bukina Faso pamba, Misri pamba, viazi mviringo, mahindi, ngano, tikiti maji na matango.

Pia Sudan na Ethiopia pamba, Kenya pamba, mahindi, viazi vitamu, muhogo na mtama. Uganda pamba, mahindi, muhogo, migomba na mpunga. Malawi migomba na pamba, eSwatini pamba, Msumbiji mahindi, Zimbabwe pamba na tumbaku na Afrika Kusini mahindi, viazi mviringo, miwa na pamba.

Kwa Tanzania utafiti ulifanyika kwenye mazao ya mahindi na muhogo, hata hivyo ulisitishwa mwaka 2021. Ni nchi chache za Afrika na nchi nyingine zinazoendelea ambazo zimeweza kupeleka teknolojia hizo za mbegu zilizoboreshwa zenye ukinzani kwa magonjwa, wadudu waharibifu na kuhimili ukame kwa wakulima wake.

Anasema sababu kubwa ni upungufu kwenye kuweka mikakati ya kujenga uelewa na ufahamu wa manufaa yatokanayo na matumizi salama ya bidhaa zitokanazo na teknolojia hiyo kwa umma.

Kuhusu matumizi ya mazao yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akiwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), alieleza kuwa wizara imekubaliana na SUA kufanyia utafiti teknolojia hiyo kwa sababu kwenye vyuo vikuu ndio makosa yote yanatakiwa yafanyike na mafanikio yaonekane.

“Na nimewaagiza Tari (Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania) kuwa sisi hatutumii GMO, lakini hatuwezi kukataa kuijua, wataalamu wa baoteknolojia wanazalishwa kwa hiyo tumetenga vituo ndani ya wizara ya kilimo viwili.

“Tari Mikocheni na kingine cha Makutupora, hivi ndio vitakuwa vinatumika Kilimo kikisimamiwa vizuri kina tija kwa mkulima na nchi. Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

1 comments

Comments are closed.