UTAFITI: Mbegu safi za muhogo huongeza asilimia 81 mavuno

 

TAFITI nchini Tanzania zimeonyesha kwamba zao la muhogo lililopandwa kwa kutumia mbegu bora zilizo safi huzaa mavuno mengi kwa ongezeko la asilimia 81 zaidi ya mavuno ya muhogo uliopandwa kwa kutumia mbegu zisizo safi.

Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo cha Kitropiki (IITA), Juma Yabeja ameyasema hayo wakati akizungumza na HabariLeo katika maonesho ya mazao yaliyofanyika katika viwanja vya taasisi hiyo kama sehemu ya program ya kongamano kubwa la chakula linaloendelea mkoani Dar es Salaam.

Amesema mbegu hizo zisizo safi wakulima hurudia kuzipana kila mwaka bila ambazo zinakuwa hazijathibitishwa na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (Tosci).

“Tafiti zilizofanywa na IITA na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kwenye Kanda za Pwani na Ziwa, mwaka jana na mwaka huu zimeonyesha kwamba matumizi ya mbegu bora za muhogo zilizothibitishwa na Tosci huongeza mavuno karibia mara mbili ukilinganisha na mbegu bora zisizo safi,

“Ambazo wakulima hurudia kuzipanda kila mwaka bila kuthibitishwa na Tosci. Aina tatu za mbegu bora zilijaribiwa na mavuno yake yalifanana,” alisema.

Amewashauri wakulima kuanzisha mashamba mapya ya muhogo kwa kutumia mbegu bora zilizothibitishwa.

Amesema mbegu hizo hupatikana kwa wakulima wazalishaji wanaosimamiwa na Tosci hapa nchini

Habari Zifananazo

Back to top button