Utamu warejea Ligi ya Mabingwa Ulaya

LIGI ya Mabingwa Ulaya inarejea leo ambapo mabingwa watetezi Manchester City wataanza kutetea ubingwa wao katika mchezo wa kwanza dhidi ya Crvena Zvezda uwanja wa Etihad.

Baada ya kukosekana kwa miaka minane, Arsenal wataanza kampeni ya mashindano hayo dhidi ya PSV kesho uwanja wa Emirates.

Manchester United pia watakuwa Allianz Arena kucheza na Bayern Munchen mchezo utakaopigwa kesho pia.

Newcastle United wanakamilisha idadi ya timu nne kutoka England watasafiri kwenda jiji la Milan nchini Italia kukabiliana na AC Milan katika mchezo wa kundi F.

Michezo mingine itakayopigwa leo Jumanne PSG dhidi ya Dortmund, Young Boys na RB Leipzig, Lazio na Atletico Madrid, Shakhtar Donetsk na FC Porto.

Barcelona dhidi ya Antwerp, Feyenoord dhidi ya Celtic, michezo hiyo pia itapigwa leo.

Kesho pia Uefa itaendelea kwa michezo mingine, Real Madrid dhidi ya Union Berlin, Galatasaray dhidi ya Copenhagen. Benfica na RB Salzburg, Braga dhidi ya Napoli.

Sevilla dhidi ya Lens, Real Sociedad na Inter Milan.

Habari Zifananazo

Back to top button