Utandawazi watajwa kuongeza magonjwa yasiyoambukiza

MKURUGENZI Msaidizi wa Magonjwa Yasiyoambukiza (MYA) Wizara ya Afya, Dk. James Kiologwe amesema utandawazi umekuwa ukichangia magonjwa yasiyoambukiza .

Utandawazi huo unajumuishwa na mabadiliko katika tafsiri ya aina ya ulaji unaofaa na tabia ya ushughulishaji mwili.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya miezi miwili kwa wanahabari kuhusu Magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

“Sasa tafsiri ya chakula bora ni kula chipsi yai na sio mbogamboga na matunda,pia tafsiri ya mtu aliyendelea anapanda bodaboda na sio kutembea kwa mguu hali imebadilika,”allmeeleza.

Amebainisha kuwa robo tatu ya watanzania hajitambui kama wanamagonjwa hayo huku asilimia 95 hufika hospitali ugonjwa ukiwa hatua ya juu hali inayofanya gharama za matibabu kuwa kubwa.

‘Mfano figo kwa mwaka kusafisha inachukua hadi milioni 36 hadi 42 ,saratani ya shingo ya kizazi ikigundulika mapema inatibika lakini mgonjwa akichelewa natumia gharama ya Sh milioni 7.6 na saratani ya matiti ikiwa hali ya juu inagharimu hadi Sh milioni 1.

Dk Kiologwe ameeleza kuwa MYA yamekuwa mzigo mkubwa kwa nchi ambapo kati ya watu 100 watu 26 wanashinikizo la damu na kati ya watu 100 watu tisa wanaugonjwa wa kisukari.

Aidha amesema kila mwaka kuna visa 11 ,Matatizo ya afya ya akili ambapo watu milioni saba wanakumbana nayo na vifo vya asilimia 30 hadi 10 vinayosababishwa na MYA.

Amesema kwa Tanzania sasa watu wanaopata magonjwa hayo wanaumri mdogo hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa huku matibabu hayo yakichukua muda mrefu na gharama kubwa.

Dk Kiologwe amewataka waandishi wa habari ambao wanapata mafunzo waweze kubobea katika eneo la MYA kwani wanamchango mkubwa katika kuelimisha na kuhabarisha jamii.

Habari Zifananazo

Back to top button