Utatuzi wa kero waipa serikali mapato

DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema limetatua kero 6000 kutoka mwaka 2019/20 hadi kufikia 10,000 kwa mwaka 2022/22 na kusaidia kuongeza pato katika mfuko wa serikali kutoka Sh bilioni 9 mwaka 2018 hadi Sh bilioni 43 kwa mwaka 2023.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 5, 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa TASAC, Nelson Mlali katika wasilisho kuhusu utekelezaji wa mafanikio ya shirika hilo wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari.

Amesema uundwaji wa nyenzo za udhibiti wa safari za majini ikiwemo utungwaji wa sheria, kanuni na miongozo imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza hali ya usalama katika safari za majini.

Akizungumzia fursa zilizopo katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji, Mlali amewataka Watanzania kuchangamkia fursa ya mahitaji ya soko la Comoro kwa kutumia usafiri wa maji kupeleka bidhaa nchini huko pamoja na uanzishwaji wa viwanda vya utengenezaji malighafi za ujenzi wa bandari rasmi za uvuvi.

Mhandisi Said Kaneko akizungumzia meli za kigeni zinazoingia nchini amesema pamoja na changamoto za wataalamu wa ukaguzi wa meli za kigeni uliopo nchini hadi sasa kuna wataalamu 16 pekee ambao wamefanikiwa kukagua meli 283 kutoka meli 39 kwa mwaka uliopita.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile ameipongeza TASAC kwa utendaji wake na kuwashauri kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa mbali mbali zinazopatikana katika sekta ya usafiri wa majini hapa nchini.

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC lilianzishwa rasmi mwaka 2018 likiwa na jukumu kuu la kusimamia usafiri kwa njia ya maji.

Habari Zifananazo

Back to top button