Utekelezaji wa TanRAP, mwelekeo mpya kukabili ajali barabarani

JITIHADA za Tanzania kukabiliana na wimbi la ajali za barabarani zinazogharimu maelfu ya watu kila kukicha, zinatarajiwa kuchukua uelekeo mpya.

Hii ni baada ya jana (Machi 02), Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia waziri wake, Profesa Makame Mbarawa kushuhudia utiaji saini makubaliano ya kuanzishwa rasmi utekelezaji wa Mpango wa Tathmini ya Barabara Tanzania (Tanzania National Roads Assessment Program – TanRAP).

Tukio hilo ni miongoni mwa tukio katika hafla ya kuhitimisha miaka miwili ya utekelezaji wa Mpango wa Hatua 10 kwa Miundombinu

Advertisement

Salama ya Barabara, mpango uliozinduliwa Machi 2021 naaliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho, huku utekelezaji wake ukitajwa kuwa wa mafanikio makubwa yatakayotumika kuutekeleza katika mataifa mengine.

Tanzania imekuwa nchi ya kwanza duniani kutumia

mpango huo ulioandaliwa na Programu ya Ushirikiano wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani (UNRSC), unaolenga kupunguza

kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani, majeruhi, ulemavu na vifo vitokanavyo na ajali hizo kwa kujenga uwezo wa ndani wa kitaasisi

kuboresha usalama wa miundombinu.

Kwa ufadhili wa pamoja wa UNRSF na Kituo cha Kimataifa cha Usalama Barabarani cha Benki ya Dunia kupitia Mfuko wake wa  Kimataifa wa Usalama Barabarani (GRSF), mradi huo pamoja na mambo mengine ulidhamiria kuhakikisha Tanzania inaanzisha

Mpango wake wa Kitaifa wa Tathmini ya Barabara (RAP) na mfumo wa mafunzo na uidhinishaji au utoaji ithibati kwa wataalamu wa utekelezaji wa mpango wenyewe. Uliwakutanisha kwa pamoja Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wakala wa

Barabara (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Umoja wa Mataifa (UN), Tume ya Uchumi ya Afrika (UNECA), Benki ya Dunia, Shirikisho la Barabara la Kimataifa (IRF), Chama cha Barabara Duniani (PIARC), Mpango wa Kimataifa wa Tathmini ya Barabara (iRAP), Shirikisho la Barabara Tanzania (TARA),

taasisi za utafiti, mashirika yasio ya kiserikali (NGOs) na wadau wa sekta hiyo. Huu ni mpango unaoweza kupangwa kulingana na hali halisi ya nchi

kiuchumi na kimaendeleo, na umebuniwa kwa njia yakuleta maarifa ya kimataifa na kuyaweka pamoja na kazi nzuri ya kuimarisha miundombinu ambayo tayari inafanyika katika kubaini mapungufu, kujenga uwezo wa kuziba mapengo hayo na hatimaye kuhakikisha barabara zinaboreshwa na kuwa salama zaidi kwa watumiaji wote wa barabara.

Utekelezaji wa mpango huo umelenga kufanikisha lengo namba tatu na nne ya Mkakati wa UN wa kuimarisha usalama barabarani na kupunguza madhara yatokanayo na ajali za barabarani kwa asilimia 50 kupitia Muongo wa kuchukua hatua kuimarisha usalama barabarani(2021–2030).

Lengo namba tatu la mkakati huo, linazitaka nchi wanachama wa UN kutilia kipaumbele uboreshaji wa miundombinu ya barabara zake kwa kuhakikisha barabara zote mpya zinazojengwa zinakuwa na hadhi

ya angalau nyota tatu, huku lengo namba nne likitaka kuboreshwa kwa miundombinu  ya zamani kuongeza usalama wa watumia barabara hususani wasafiri kwa angalau asilimia 75 ifikapo mwaka 2030.

MAANA YA KUHITIMISHWA MRADI HUU KWA TANZANIA

Moja kati ya mambo ambayo Jumuiya ya Kimataifa inaondoka nayo kufuatia kukamilika kwa mradi huu ni ripoti nzuri ambayo pamoja na mambo mengine, itaiambia Jumuiya ya Kimataifa kuwa haikukosea kuiteua Tanzania kama nchi ya kufanya majaribio ya utekelezaji wa mradi huu.

 

Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo yangeweza kuifanya Tanzania kufanya vibaya katika utekelezaji wa jaribio hili, miongoni ni asilimia kubwa ya Watanzania kutokuwa na utamaduni wa kupenda mambo yenye kuhusiana na usalama barabarani na ukweli kuwa hakuna mahali pengine ambako umeshawahi kutekelezwa ili kupata uzoefu.

Hata hivyo, hali imekuwa ni tofauti kwani utekelezaji wake umekuwa wa mafanikio makubwa huku Tanzania ikigeuka kuwa nchi itakayotumiwa na wengi kama sehemu ya kupata uzoefu wa namna bora ya kutekeleza miradi ya aina hii kwenye mataifa yao.

Idadi kubwa ya watu waliojitokeza kwa ajili ya kusoma masomokuhusiana na uhandisi wa usalama barabarani, wakiwemo watu ambao hawakuwa na elimu ya msingi juu ya masuala hayo, imekuwa kiashiria kimojawapo si tu cha kuwa Watanzania wengi sasawanaanza kuupa usalama barabarani kipaumbele, bali pia kielelezo kuwa kumbe

hata wasiojihusisha na masuala ya utengenezaji wa barabara kwa namna yoyote ile, wanaweza kusoma masomo hayo na kuwa wataalamu wazuri katika kusaidia mataifa na jamii kuwa salama barabarani.

Miongoni mwao ni mwandishi wa makala haya ambaye licha ya kuwa mwanahabari kitaaluma alihitimu mafunzo hayo na kuwa miongoni mwa watu 19 ambao walitunukiwa ithibati za kimataifa katika upembuzi wa barabara, utoaji alama na hadhi ya nyota za ubora wa barabara pamoja na eneo la uchambuzi, uandaaji na utoaji taarifa kuhusu tathmini za usalama wa barabara.

Zaidi ya watu 800 walijisajilikwa mafunzo hayo yaliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na zaidi ya nusu walisoma angalau kozi tatu kati ya zaidi ya kozi 12 zilizotolewa.

Aidha, ushirikiano wa taasisi za ndani katika kufanikisha kuanzishwa kwa TanRAP, kuanzia hatua za awali za kubuni muundo, mfumo wa uendeshaji na hatimaye sasa makubaliano ya utekelezaji wake ni kiashiria kingine cha mafanikio makubwa ya utekelezaji wa mpango huowa Hatua Kumi.

Kutokana na maelezo hapo juu, ni wazi kuwa kuhitimishwa kwa utekelezaji wa mradi wa majaribio wa Mpango wa Hatua Kumikwa Miundombinu Salama ya Barabara, kunamaanisha kuwa Tanzania sasa ina wataalamu zaidi wenye elimu, ujuzi na utaalamu kuhusiana na usalama barabarani na kama mmoja wa wanachama wa UN walioridhia kutekeleza mkakati wa UN wa kupunguza madhara ya ajali kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030, kupitia Muongo wa Pili wa UN wa Kuimarisha

Usalama Barabarani, basi iko tayari kutumia rasilimali hii ya wataalamuwa ndani kufanikisha hilo.

NINI KINAPASWA KUFANYIKA

Moja kati ya changamoto zinazotatiza suala la usalama barabarani nchini ni ukweli kuwa ni jambo ambalo licha ya umuhimu wake, limekuwakama halina mwenyewe. Kumekuwa na mamlaka zaidi ya moja ambazo zinasimamia usalama barabarani, huku zikiwa hazina ushirikiano katika kuandaa na kutekeleza vipaumbele vya kuimarisha usalama barabarani Changamoto hii ni miongoni mwa changamoto ambazo timu itakayokuwa ikiunda TanRAP, itatakiwa kuifanyia utafiti wa haraka na kutoa mapendekezo yatakayosaidia serikali kuona namna gani inakuwa na taasisi kiongozi katika masuala ya usalama barabarani.

Hili litasaidia utekelezaji endelevu wa hatua za uimarishaji usalama barabarani sanjari na ufanyaji tathmini wa juhudi za wadau katika masuala yote yenye kugusa usalama barabarani. Nyingine itakayotakiwa kufanyiwa kazi haraka ni kuibua miradi ya kuimarisha usalama barabarani na wahisani wa kufadhili utekelezajiwa miradi hiyo.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo iko katika hatua za kujiimarisha kimiundombinu huku pia ikijiimarisha katika nyanja nyingine za kimaendeleo, ufinyu wa bajeti kwa masuala yenye kuhusu usalama

barabarani ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Mifano  ya hii ni ujenzi wa barabara.

nyingi za kisasa ambao umekuwa ukifanyika lakini zikawa zinakosa vitu vya msingi vya kiusalama. Ni jukumu ambalo wataalamu waliojengewa uwezo na kupatiwa elimu kupitia Mpango wa Hatua Kumi kwa Miundombinu Salama ya Barabara, watatakiwa kulifanyia kazi kwa haraka. Masuala kama ya kuandaamfumo wa utoaji elimu ya usalama barabarani tangu ngazi za awali za mifumo rasmi ya elimu, ushirikiano na wadau wakiwemo wanahabari katika kuhakikisha kunakuwa na wanahabari waliobobea kwenye usalama barabarani, haya ni masuala ambayo yanaweza kufanyiwa kazi na TanRAP, ili kuongeza tija na ufanisi katika juhudi za serikali kwenye kuimarisha sekta ya miundombinu.

Kwa upande mwingine, serikali ina wajibu wa kuhakikisha inawapa nafasi  ya upekee wataalamu 19 waliohitimu vyema mafunzo yao, ili kuwawezesha kuendelea kufanyia kazi kile walichojifunza kwa manufaa ya taifa lao.

Kama ambavyo tumeifanya Tanzania kuwa sehemu ya kujifunza namna  utekelezaji wa Mpango wa Hatua Kumi unaweza kufanya kazi, ndivyo ambavyo ninaamini serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, itawezesha nchi kuwa sehemu ya wengine kujifunza namna ambavyo  imetekeleza yale yaliyotokana na mpango huo.

Mwandishi ni Balozi wa

Usalama Barabarani kupitia

RSA Tanzania ambao ni

washiriki wenza kwenye

TanRAP.

Simu 0767412176, msangirs@

gmail.com

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *