UTEUZI: Mkurugenzi Tanesco apelekwa TTCL
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano (TTCL).
–
Kabla ya iteuzi huo, Chande alikuwa Mkurugenzi wa Mtendaji Mtendaji wa Shirika la Umeme ( TANESCO).
–
Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Peter Ulanga aliyekuwa Mkurugenzi TTCL atapangiwa kazi ingine.
–
Rais Samia pia amemteua Mhandisi Gissima Nyamo Hanga Mkurugenzi wa Shirika la Umeme ( TANESCO ), Nyamo aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini REA.
–
Aidha, Dk Erasmus Fabian Kipesha ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kabla ya uteuzi huo Dk Kipesha alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA).